Sessions kuhojiwa na Baraza la Seneti maswali magumu

Jeff Sessions

Mwanasheria mkuu wa Marekani Jeff Sessions Jumanne atatoa ushahidi hadharani mbele ya jopo la wajumbe wa baraza la senate.

Wajumbe hao wanatarajiwa kumuuliza maswali magumu kuhusu uhusiano wake na balozi wa Russia pamoja na iwapo alihusika kumfukuza kazi kwa mkuu wa idara ya upelelezi ya FBI James Comey.

Kikao hicho cha kamati ya upelelezi katika baraza la senate ndiyo hatua ya karibuni katika uchunguzi unaoendelea kuhusiana na madai ya Russia kuingilia uchaguzi wa rais wa marekani mwaka uliopita.

Sessions alijiondoa kwenye uchunguzi wa FBI mwezi machi baada ya kukiri kuwa alizungumza mara mbili na balozi wa Russia Sergey Kislyak miezi kadhaa kabla ya uchaguzi kufanyika mwezi novemba.

Wakati wa kuidhinishwa kwake Januari, Sessions alikanusha kukutana na afisaa yeyote kutoka Russia.