Kufuatia kupatikana kwa mwanaharakati wa chama cha Upinzani cha Chadema, Mdude Nyagali, baada ya kutekwa na watu wasiojulikana siku tano zilizopita, viongozi wa chama hicho, sasa wanaitaka serikali kutoa taarifa kamili kuhusu ni nani aliyemteka mwanasiasa huyo.
Mdude alipatikana jana usiku akiwa na majeraha kadhaa, na anaendelea kupokea matibabu katika hospitali moja ya mkoa wa mbeya.
VOA imezungumza na afisa wa chama cha Chadema katika mji wa Mbeya, John David Mwambigija, na kuanza kwa kumuuliza mwanaharakati huyo alipatikana katika mazingira gani?
Your browser doesn’t support HTML5