Serikali tayari imechukua hatua kutafuta wale waliohusika na kuchoma shule hiyo, amesema Waziri wa Elimu Fred Matiang'i Jumatatu.
Pia waziri amesema kuwa Idadi ya vifo katika ajali hiyo imeongezeka kufikia tisa.
Dr Matiang’i amesema msichana mmoja mwengine ambaye amelazwa hospitali ya Nairobi Women wakijaribu kuokoa maisha yake alifariki dunia kutokana na majeraha ya moto Jumapili.
Baada ya kifo cha mwanafunzi huyo bado kuna wanafunzi wengine wawili katika kitengo cha wagonjwa waliokuwa na hali mbaya.
Dr Matiang’i ameongeza kuwa wanafunzi wote hapo shuleni wamepatikana, na kuwa uvumi wa kuwa baadhi ya wanafunzi wamepotea sio kweli.
“Wakati nikiwa hapo shuleni nimeagiza kuwa wanafunzi wote waruhusiwe kuondoka shuleni pale watakapokuja kuchukuliwa na wazazi wao.
Katika tukio hilo la moto Jumamosi wanafunzi 51 walijeruhiwa na wamepelekwa Hospitali ya Nairobi Women akiwa na majeraha ya viwango mbalimbali.
Jumla ya wanafunzi 40 walitibiwa na kuruhusiwa kurudi nyumbani wakati wengine 11 walilazwa hospitali na kati yao watatu walikuwa na majiraha mabaya sana.
Wanafunzi wanane wamekufa Jumamosi kufuatia tukio hilo la moto.