Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 19:51

Uganda yapatwa na taharuki kufuatia mauaji ya wanawake 28


Misitu iliyoko katika eneo karibu na Entebbe, Uganda.
Misitu iliyoko katika eneo karibu na Entebbe, Uganda.

Mauaji ya wanawake nchini Uganda limekuwa jambo ambalo limesababisha wasiwasi sio tu kwa wakaazi wa mji wa Entebbe wilayani Wakiso, karibu na mji mkuu wa Kampala, bali pia kwa maafisa wa polisi hasa viongozi wakuu, bila ufumbuzi wa mhusika anayefanya mauaji hayo.

Mauaji ya wanawake nchini Uganda limekuwa jambo ambalo limesababisha wasiwasi sio tu kwa wakaazi wa mji wa Entebbe wilayani Wakiso, karibu na mji mkuu wa Kampala, bali pia kwa maafisa wa polisi hasa viongozi wakuu, bila ufumbuzi wa mhusika anayefanya mauaji hayo.

Wanawake wa umri wa ujana, wamekuwa wakipatikana wameuawa, na miili yao kutupwa, ikiwa imeingizwa vijiti katika sehemu zao za siri.

Uchunguzi wa madaktari umekuwa ukiarifu kwamba wote waliokutwa wameuwawa, huuawa kwa kunyongwa vipimo vikionyesha kwamba hubakwa kabla ya kunyongwa, na pia vijiti huingizwa katika sehemu zao za siri na kisha kunyongwa hadi kufa.

please wait

No media source currently available

0:00 0:05:01 0:00

Miili yao, hutupwa vichakani.

Kwa muda wa miezi miwili, mauaji hayo sasa yametiliwa mkazo, wakuu serikali wakitaka mhusika kukamatwa, idadi ya wanawake waliouawa hadi sasa imefikia 28.

Japo kuna maswali chungu nzima kuhusu sababu ya wauaji kuwalenga wanawake, mkuu wa polisi Generali Kale Kayihura anahusisha mauaji hayo na ushirikina kwa lengo la kupata utajiri.

“Kuna mshukiwa ambaye amekiri kwamba ameua wasichana 8 katika mtaa wa Nansana na kwamba alilipwa kufanya hivyo na mtu aliyetaka kupata damu. Huyo aliyetaka damu naye tumemkamata. Tunawasihi waandishi wa habari nao kutusaidia katika upekuzi,” amesema Kayihura.

Kulingana na Kayihura, mauaji ya wanawake katika sehemu hiyo, ni suala linalo wakera maafisa wa polisi, ambao licha ya kutumia mbinu za kisasa kuwasaka wahusika, polisi hawajafanikiwa.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni naye ameelezea kukasirishwa na mauaji hayo, hasa ikitiliwa mkazo kwamba mji wa Entebbe ndio ilipo ikulu ya rais, na inatarajiwa kwamba usalama katika eneo hilo ni wa hali ya juu na kuaminika.

Wanawake wanaouawa wana umri wa kati ya miaka 20 na 35.

“Tumeweza kukamata zaidi ya washukiwa 36. Wamekamatwa katika maeneo mbali mbali ya Katabi na Nansana. Katika upelelezi wetu, matamshi yao yanaonekana kukaribiana. Tumemkamata pia mshukiwa tunayeamini ni mhusika mkuu katika mauaji haya,” mkuu wa polisi anasema.

Mauaji ya wanawake pia yameripotiwa katika manispaa ya Nansana, wilayani Wakiso, licha ya mkuu wa polisi jenerali Kale Kayihura kukita kambi katika eneo hilo na kufanya mabadiliko makubwa katika uongozi wa polisi katika eneo hilo yakiwa pamoja na kubadilisha makamanda wake wote.

Jenerali Kayihura pia amekuwa akitembelea maeneo ya Entebbe na Nansana mara kwa mara.

Zaidi ya watu 16 wakiwemo rafiki wa kimapenzi wa wanawake hao, waume wao, na waganga wamekamatwa.

“Napenda kuihakikishia nchi kwamba tutafaulu kuwanasa wahusika. Tumekumbana na visa vigumu vya uvunjaji wa sheria na tumefanikiwa. Tatizo ni kwamba huwa tunapata tu maiti bila shahidi.”

Suala hili sasa limedhihirika kuwakosesha wabunge amani. Spika wa bunge la Uganda bi Rebecca Kadaaga, sasa anataka taarifa kamili kutoka kwa waziri wa usalama,Henry Tumukunde na mwenzake wa mambo ya ndani jeneraliJeje Odong kulieleza bunge sababu za kuuawa kwa wanawake, nanani mhusika.

Katika taarifa ya maandishi, Bi Kadaaga anataka mawaziri hao kumjibu haraka iwezekanavyo, na bunge kujadili swala hilo mwezi Septemba.

Miili ya wanawake wanaouawa, hupatikana ikiwa tayari imeanza kuoza.


XS
SM
MD
LG