Sera ya Biden kwa China: Je, fanya mazungumzo wakati unajiandaa kupambana?

Rais wa Marekani Joe Biden afanya mazungumzo na mwenzake wa China Xi Jinping kwa njia ya mtandao, White House Jumatatu Nov. 15, 2021, Waziri wa Fedha Janet Yellen, kulia, na Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken wakisikiliza. (AP Photo/Susan Walsh)

Mazungumzo ya kijeshi kati ya China na Marekani yaliyofanyika sambamba na kuongezeka kwa bajeti ya ulinzi mwezi huu ni kiini muhimu cha sera ya Rais Joe Biden kwa China – zungumzeni na jiandaeni kupambana kwa wakati mmoja – wachambuzi wanaamini.

Baraza la Seneti la Marekani lilipiga kura Jumatano kwa maelezo ya sheria ya kuidhinisha ulinzi wa kitaifa (NDAA) inayopitisha dola bilioni 770 kwa matumizi ya ulinzi, dola bilioni 25 zaidi ya kiwango alichokuwa ameomba Biden na ikiwemo dola bilioni 7.1 kwa ajili ya juhudi za Kulilinda eneo la Pacific yenye lengo la kudhibiti upanuzi wa China.

Kuanzia Jumanne hadi Alhamisi, wawakilishi kutoka Kikosi cha Indo-Pacific cha Marekani, jeshi la majini na jeshi la anga walikutana kwa njia ya mtandao na wenzao wa upande wa China wa jeshi la anga na majini kwa mazungumzo ili kuhusu usalama katika eneo la majini lenye mvutano.

“Jeshi la Marekani, wanafanya kile wanachoweza, kama vile kuhakikisha uhuru wa operesheni za majini katika eneo la bahari ya South China, lakini pia wanahakikisha kuna mipaka, wanaendelea kuweka njia za mawasiliano wazi na Wachina,” amesema Aaron Rabena, mtafiti katika Taasisi ya Maendeleo ya Njia za Majini katika eneo la Asia-Pacific huko mjini Manila.

SOUTH CHINA SEA (Nov. 20, 2021) Manuari ya Arleigh Burke-class guided-missile destroyer USS Milius (DDG 69) ikiwa katika eneo la Bahari ya South China Nov. 20, 2021.

Washington iliongeza mwaka 2019 idadi ya manuari zinazopita katika eneo la bahari ya South China kufikia 10 kwa mwaka, idadi iliyorejewa mwaka 2020. Maafisa wa Marekani wanaeleza upitaji huo kama “Uhuru wa operesheni za usafiri wa majini.”

China na Marekani wako katika kile wanazuoni wanakieleza ni “ushindani wa nguvu kubwa,” huku Washington hasa ikilenga kudhibiti upanuzi wa katika bahari ya Mashariki na Kusini mwa China ambako Marekani inazichukulia nchi za karibu ya eneo hilo na washirika wa kisiasa.

Biden ataendelea na ushindani huo lakini ana matumaini ya kuzuia kuzuka kwa ghasia, wachambuzi wanaeleza.

Mkutano wa Rais Joe Biden na Rais Xi Jinping kwa njia ya mtandao.

Maandiko ya mswaada wa NDAA uliopitishwa Jumatano ulijumuisha taarifa ya uungaji mkono wa bunge kwa ulinzi wa Taiwan na kupiga marufuku manunuzi ya wizara ya ulinzi ya bidhaa zozote zinazo zalishwa kwa kutumia nguvu kazi ya kulazimishwa kutoka mkoa wenye Waislam wengi wa Xinjiang. Sheria hiyo inahitaji kusainiwa na Biden.

Mazungumzo ya kijeshi, mchakato ulioanza mwaka 1998, yalifanyika ili kupunguza hatari na kuboresha “operesheni za kiusalama” katika anga na bahari, kikosi cha Indo-Pacific cha Marekani kimesema katika taarifa yake. Maafisa wa Marekani na China wakati huu walijadili “uweledi” na kuhakiki matukio “yanayohusu usalama,” taarifa ya Ijumaa ilisema.

China inasema eneo mraba la kilomita milioni 3.5, lenye rasilmali zenye utajiri katika bahari ya South China ni mali yake, ikivutana na madai ya nchi zenye uwezo dhaifu wa kijeshi za Brunei, Malaysia, Ufilipino, Taiwan na Vietnam.

Ramani ya Bahari ya South China

Manuari za kivita za Marekani pia hupita katika mlango wa bahari wa Taiwan, ikiwa ni onyo dhidi ya China isijaribu kukishambulia kisiwa kinachojitawala, ambacho China inadai ni miliki yake.

Usimamizi wa migogoro, kama vile “Itifaki za meli kwa meli” na mawasiliano ya moja kwa moja, ni kipaumbele cha juu cha jeshi la Marekani kwa China, amesema Gregory Poling, mkurugenzi wa Juhudi za Uwazi za Eneo Bahari la Asia chini ya Kituo cha Tafiti za Kimkakati na Masuala ya Kimataifa chenye makao yake Washington.