Kwa mijubu wa shirika la habari la Reuters, ziara hiyo anafanyika kukiwa na tetesi za uwekezaji mkuwa wa Saudia, nchini Misri ambayo imepokea fedha nyingi mwaka huu zikiwemo dola bilioni 35 kutoka mfuko wa UAE wa ADQ.
Ziara ya mwisho rasmi ya Mohammed Bin Salman nchini Misri ilifanyika 2022. Saudi Arabia ambayo imekuwa ikitoa misaada ya Misri katika miaka ya nyuma imeashiria kubadili mikakati na badala yake kuanza kuwekeza moja kwa moja kinyume na kutoa misaada kwa washirika wake.
Mwezi uliopita, waziri mkuu wa Misri alisema kuwa Saudi Arabia inapanga kuwekeza dola bilioni 5 nchini mwake, tofauti na fedha ambazo zilikuwa zimehifadhiwa kwenye Benki kuu wa Misri. Baadhi ya uwekezaji ni pamoja na maeneo mawili ya kitalii kwenye ufukwe wa Bahari ya Shamu, pamoja na kwenye peninsula ya Sinai, yote yakiangalia upande wa pili wa Saudia Arabia.