Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na White House, wakati ambapo watu wengi wanaungana pamoja kusherehekea mwezi mtukufu wa Ramadhan, Rais Trump na mkewe Melania wana matumaini kuwa mwezi huu utakuwa wa baraka.
Taarifa imesema kuwa Marekani imebarikiwa kuishi kwa mujibu wa katiba ambayo inaheshimu uhuru wa dini na inaheshimu uhuru wa kuabudu wa kila mwananchi. Katiba yetu inahakikisha kuwa waislamu wanaweza kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa mujibu wa imani yao ya dini na bila ya kuingiliwa na serikali.
Wakati wa mwezi huu wa Ramadhan, Waislamu wanasherehekea kuteremeshwa Quran tukufu kwa Mtume Mohammed. Wengi wanaadhimisha mwezi huu kwa kufunga, kufanya vitendo vyema, kusali na kusoma Quran.
Ramadhan ni wakati wa kujitathmini kwa azma ya mtu kujifahamu kwa undani nafsi yake na kuwa na dhana ya kushukuru kwa Baraka nyingi ambazo wanazipata kutoka kwa Mwenyenzi Mungu.
Katika azma hii ya kushukuru na kujitathmini, wale wanaoadhimisha mwezi mtukufu wa Ramadhan wanasema kuziimarisha jamii zetu, kuwasaidia wale wenye shida, ni mfano mzuri wa jinsi ya kuishi maisha safi kwa waumini wa dini.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa Ramadhan inatukumbusha utajiri wa Waislamu ukiongezea na dini katika maisha ya Marekani. Nchini Marekani, tumebarikiwa kuishi kwa mujibu wa katiba ambayo inahamasisha uhuru wa dini na kuheshimu dini.
Katiba ya Marekani inahakikisha kuwa Waislamu wanafunga Ramadhan kwa mujibu wa misingi ya dini na bila ya kuingiliwa na serikali, taarifa imesema.
Kwa kufanya hivyo katiba pia inatoa fursa mbali mbali kwa Wamarekani wote kuelewa nafasi ya binadamu.