RMS Titanic Inc, yenye makao yake kwenye jimbo la Georgia ina haki za kuokoa meli hiyo iliozama kwenye bahari ya Atlantic Kaskazini 1912. Safari imeanza Ijumaa kuanzia kwenye mji wa Providence, Rhode Island, ya mwisho ikiwa ilifanyika 2010. S
afari hiyo inafanyika wakati jamii ya watafiti wa chini ya bahari wakiwa wangali wameshtushwa na ajali ya chombo kilichoporomoka kikielekea kwenye meli hiyo Juni mwaka uliopita. Wote waliokuwa kwenye chombo hicho walikufa akiwemo Paul Henri Nargoelet, ambaye alikuwa mkurugenzi mkuu wa utafiti kwenye kampuni ya RMS.
Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo Jessica Sanders amesema kuwa sasa ndiyo watafanya hata zaidi licha ya kifo cha Nargoelet, ambaye wengi kwenye kampuni hiyo walimuita Mr Titanic.