Rwanda yakumbuka mauaji ya halaiki

Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat, Rais wa Rwandan Paul Kagame, mkewe Jeannette Kagame and Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya Juncker, wakiwasha moto wa matumaini katika kituo cha kumbukumbu ya mauaji ya halaiki huko Gisozi, Kigali, Apr. 7, 2019.

Rwanda inaanza Jumapili siku 100 za maombolezi ya zaidi ya vifo vya watu 800,000 waliopoteza maisha wakati wa mauaji ya halaiki Aprili 7, 1994, miaka 25 iliyopita.

Kila April 7, wananchi wa Rwanda wanaadhimisha kumbukumbu ya mauaji ya halaiki ambayo yaliacha maelfu ya watu wameuawa, na kauli mbiu za kumbukumbu hii inasema “Isereje Kamwe Tena.” Suala la kuzuia mauaji ya halaiki yasitokee tena litazungumziwa wakati wa maadhimisho hayo.

Rais Paul Kagame ataizindua wiki ya kumbukumbu kwa kuwasha mwenge katika eneo maalum ambako mauaji hayo yalitokea

Makaburi

Eneo hilo mjini Kigali, zaidi ya watu 250,000 wanaaminika wamezikwa, wengi wao wakiwa ni kutoka jamii ya Watusti.

Rais Kagame pia atakuhutubia katika kituo cha mikutano cha mjini Kigali. Kiasi ya viongozi 10 wataweka mashada ya maua katika eneo hilo.

Ubelgiji

Watakao hudhuria kumbukumbu hiyo ni pamoja na Waziri Mkuu wa Ubelgiji, Charles Michel.

Ujerumani

Wakati huo huo, vyanzo vya habari nchini Rwanda vimeripoti kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Heiko Maas amesema mauaji ya halaiki ya Rwanda yanapaswa kuchukuliwa kama onyo kwa vizazi vijavyo.

Simulizi ya manusura wa mauaji ya halaiki

“Nilikuwa na watoto wangu wakati wanakufa.” Amesema Lydia Uwamwezi, akisimulia siku mia moja za mauaji ya halaiki yalioanza miaka 25 zilizopita siku ya Jumapili Rwanda.

“Kuna mto wa maji kati ya maeneo ya Kigina na Nyarubuye. Huko ndiko kundi kubwa la hao wahalifu lilipotupeleka. Walikuwa wamechoka kutumia mapanga, hivyo basi waliwatupa watoto wangu ndani ya ziwa.

Watoto wake watupwa ziwani

Uwamwezi hivi sasa ana miaka 46, ambaye alisalimika. Akiwa amekata tamaa, alitupa mbeleko aliokuwa anambeba mtoto wake ndani ya ziwa hilo ambalo watoto wake walitupwa na kuzama. Washambuliaji wa Kihutu waliutoa kutoka ziwani na baada ya hapo kumuingilia kingono mara kadhaa, wakimwambia lazima awazalie watoto wa Kihutu kufidia watoto wake wa Kitutsi ambao walikuwa wameshauawa.

Uwamwezi pia alimpoteza mume wake na makazi yake siku zote hizo. Hakuweza kuolewa tena au kupata watoto wengine. Baada ya serikali kutoa mafunzo ya maridhiano, amewasamehe waliokuwa wamemfanyia vitendo hivyo vya unyama.

“Iwapo utakuwa na chuki moyoni, huwezi kuendelea kuishi vizuri na majirani zako,” amesema mwanamke huyo.

Mafunzo ya maridhiano na kusameheana

Hivi leo watu hawa wanaishi pamoja, Watutsi na Wahutu, wakati mmoja walikuwa katika makundi kinzani ya mauaji hayo ya halaiki. Hivi leo wanaishi kama majirani katika nchi ambapo huduma za afya zinatolewa, mitaa inasafishwa na serikali zinawahimiza watu kusahau tafauti zao za kikabila na kujihisabu kuwa wao ni raia wa Rwanda.

Umoja wa Mataifa unafanya siku ya kumbukumbu kila mwaka. Tangu wakati huo wa mauaji ya Rwanda, matukio ya mauaji ya halaiki yametokea huko Bosnia, Sudan na Myanmar.