Tishio kwa usalama wa chakula na "vita vya maneno" na Russia juu ya vikwazo vilivyowekwa na nchi za Magharibi dhidi ya Moscow kwa sababu ya mashambulizi yake nchini Ukraine vitatawala mazungumzo ya mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya nchini Luxembourg, siku ya Jumatatu.
"Russia iligeuza Bahari ya Balck Sea kuwa eneo la vita, ikizuia usafirishaji wa nafaka na mbolea kutoka Ukraine lakini pia kuathiri usafirishaji unaofanywa na wafanyabiashara wa Russia, alisema.
Aliongeza kwamba vikwazo vilivyowekwa na jumuiya ya umoja wa ulaya "havizuii Russia kusafirisha bidhaa zozote za kilimo, malipo ya mauzo ya nje ya Russi,a au utoaji wa mbegu, mradi tu watu au taasisi zizlizowekewa vikwazo hazihusiki."
Alisema Umoja wa Ulaya unashirikiana kwa karibu na Umoja wa Mataifa juu ya suala hili, na EU na nchi wanachama wake, wako tayari kufanya linalohitajika kufikia lengo hilo.
"Tunatumai kuwa suluhu inaweza kupatikana katika siku zijazo. Kutofanya hivi kunatishia kusababisha janga la chakula duniani," alionya afisa huyo mwandamizi.