Wizara ya ulinzi ya Russia Jumamosi imesema wanajeshi wa Russia wamedhibiti kijiji cha Nadiya katika mkoa wa mashariki mwa Ukraine wa Luhansk na kutungua makombora manane yaliyotengezwa Marekani aina ya ATACMS.
Reuters haikuweza kuthibitisha ripoti hizo kutoka uwanja wa mapigano.
Wizara hiyo imesema mifumo ya ulinzi ya Russia ilitungua ndege 10 zisizo na rubani za Ukraine katika eneo la Russia Jumamosi asubuhi, zikiwemo tatu katika mkoa wa kaskazini wa Leningrad.
Shughuli za kuwasili na kuondoka kwa ndege zilisimamishwa kwa muda Jumamosi asubuhi katika uwanja wa ndege wa Pulkovo wa mji wa St Petersburg.