Kuingia kwake katika kinyang’anyiro cha urais kunabadilisha mwelekeo wa ushindani kuwania uteuzi wa Republican, kwa kuwa kuna uwezekano ataibuka kuwa mpinzani mkubwa sana wa rais wa zamani Donald Trump . Mgombea atakayeteuliwa atachuana na Rais Joe Biden , mdemocrat katika uchaguzi mkuu wa Novemba mwaka kesho.
DeSantis mwenye umri wa miaka 44 pia anapanga kuwasilisha nyaraka katika tume ya uchaguzi akitangaza rasmi ugombea wake, wafanyakazi wake wamesema.
Musk, mkurugenzi mkuu wa Tesla na Twitter akiwa na wafuasi milioni 140 katika twitter amesema kutokea kwake katika tukio hilo sio kumuidhinisha lakini litaonyesha nia yake ya kufanya utaratibu huo kuwa sawia zaidi.
Leo pia Desantis atafanya Mkutano na wachangiaji wake wakubwa katika hoteli ya Miami, ambako watazindua rasmi juhudi zake za uchangishaji.