Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 12:59

Tim Scott, Seneta pekee mweusi wa chama cha Republikan, atangaza atawania urais


Election 2024 Scott
Election 2024 Scott

Tim Scott alitangaza Jumatatu kuwa anawania uteuzi wa chama chake,  ili kugombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2024, akijitosa kwenye uwanja wa wapinzani wanaotaka kumng'oa mamlakani Rais wa Joe Biden, wa chama cha Demokratik.

Scott, mwenye umri wa miaka 57, alitangaza nia yake katika katika chuo kikuu cha Charleston Southern, kilicho katika jimbo analowakilisha.

Kwa tangazo hilo, Scott aliongeza jina lake kwenye orodha ya wagombea wa Republican ambayo kura za maoni za kitaifa zinaonyesha inaongozwa na Rais wa zamani Donald Trump, ambaye anatafuta tikiti ya kurejea White House, baada ya kupoteza ombi uchaguzi wa mwaka 2020 kwa Biden.

Scott aliteuliwa kuwakilisha South Carolina kwenye seneti kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2012 na Gavana wa wakati huo wa jimbo hilo, Nikki Haley, ambaye mwenyewe anatafuta uteuzi wa chama chake Republican, ili kugombea urais.

Kura za maoni za kitaifa za wapiga kura wa chama cha Republikan zinaonyesha wote Haley, balozi wa zamani wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, na Scott, wakiwa na usfuasi mdogo, wakiwa nyuma ya Trump na Gavana wa Florida, Ron DeSantis, ambaye mwenyewe anatarajiwa kujiunga rasmi kwenye kinyang'anyiro chahicho baadaye wiki hii.

XS
SM
MD
LG