Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 01:01

Marekani: Viongozi wanne wa kundi la mrengo mkali wa kulia wapatikana na hatia ya kula njama ya uchochezi


Kiongozi wa zamani wa kundi la Proud Boys, Henry "Enrique" Tarrio.
Kiongozi wa zamani wa kundi la Proud Boys, Henry "Enrique" Tarrio.

Baraza la Mahakama mjini Washington limemtia hatiani kiongozi wa zamani wa kundi la wanamgambo wa mrengo wa kulia la Proud Boys na washirika wake watatu kwa kula njama ya uchochezi kwa jukumu lao katika shambulizi baya dhidi ya Bunge la Marekani tarehe 6 Januari mwaka wa 2021.

Kiongozi wa zamani wa Proud Boys Enrique Tarrio na viongozi wa matawi ya kundi hilo hapa Marekani Joe Biggs, Ethan Nordean na Zach Rehl, walipatikana pia na hatia Jana Alhamisi ya kula njama ya kulizuia Bunge kurasmisha ushindi wa Joe Biden dhidi ya Donald Trump katika uchaguzi wa rais wa mwaka wa 2020.

Lakini baraza hilo la mahakama halikuweza kufikia maamuzi kuhusu mashtaka ya kula njama dhidi ya mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo, Dominic Pezzola. Pezzola ni mwanajeshi wa zamani na bondia ambaye alijiunga na kundi la Proud Boys baada ya uchaguzi wa 2020 lakini hakuwa na cheo chochote cha uongozi katika kundi hilo.

Washtakiwa wote watano wanakabiliwa na mashtaka ya makosa tisa yanayohusiana na kuzuia Bunge na maafisa wa serikali kuu kutekeleza majukumu yao.

Uamuzi huo ni ushindi mkubwa kwa wizara ya sheria ya Marekani wakati inachunguza kesi hiyo ya shambulizi baya ambalo lilisababisha vifo vya watu watano, kujeruhi zaidi ya maafisa 100 wa polisi na kupelekea uchunguzi mkubwa wa uhalifu katika historia ya Marekani.

XS
SM
MD
LG