Kila shirika la habari lilifanya uchunguzi na wataalam wa nje kukagua rekodi za video, picha za satelaiti, ushuhuda wa mashahidi na vipande vya silaha, na kuhitimisha kuwa shambulizi hilo lilikuwa la mizinga 120, mizinga inayotumiwa na jeshi la Israeli pekee.
Shambulio hilo lilitokea Oktoba 13 wakati waandishi hao walipokusanyika karibu na kijiji cha mpakani cha Lebanon cha Alma al-Chaab ili kurekodi video ya maeneo ya karibu ambapo kumekuwa na mapigano ya mpaka kati ya jeshi la Israel na wapiganaji wa Palestina.
Reuters na AFP zilisema waandishi hao walitambulika wazi kuwa ni wanaandishi wa habari wakiwa wamevalia jaketi na Kofia .
Shambulizi la awali lilipiga kundi hilo, likifuatiwa haraka kwa sekunde, mashirika ya habari yalisema. Mwandishi wa habari wa Reuters, Issam Abdallah aliuawa, huku wenzake wawili wa Reuters na mwandishi wa habari wa AFP wakiwa miongoni mwa waliojeruhiwa.
Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la Reuters na AFP.