Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, Jumatatu ameelezea wasiwasi wake mkubwa kuhusu kuanza tena kwa mapigano kati ya Israel na Hamas, ikijumuisha ufyatuaji wa roketi wa Hamas kwa Israel na kuongezwa kwa mashambulizi ya anga na operesheni za kijeshi za ardhini za Israel katika eneo la kusini mwa ukanda wa Gaza.
“Umoja wa Mataifa unaendelea kuviomba vikosi vya Israel kuepuka hatua zaidi zitakazozidisha hali ya janga la kibinadamu huko Gaza na kuwaepusha raia na mateso zaidi,” msemaji wa Umoja wa Mataifa, Stephane Dujarric amesema katika taarifa yake.
Ameongeza kusema raia ikiwa pamoja na wafanyakazi wa afya, waandishi wa habari na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa, na miundombinu ya kiraia lazima ilindwe wakati wote. Guterres alitoa wito kwa pande zote kuheshimu wajibu wao chini ya sheria ya kimataifa ya kibinadamu na kusisitiza wito wake wa kusitisha mapigano.
Forum