Rais Biden atuma salam za rambirambi kwa Mfalme wa Morocco

Rais wa Marekani Joe Biden akiwa Ikulu ya Marekani huko Washington, Septemba 17 2023. Picha na REUTERS/Evelyn Hockstein.

Rais wa Marekani Joe Biden ilizungumza na Mfalme Mohammed wa Sita wa Morocco siku ya Jumatatu, kutoa salaam za rambirambi kufuatia tetemeko kubwa la ardhi lililoikumba nchi hiyo iliyoko Afrika Kaskazini mapema mwezi huu, Ikulu ya Marekani ilisema katika taarifa yake.

Viongozi hao wawili walijadili utayari wa Washington kusaidia katika juhudi za kufufua, ilisema taarifa hiyo.

Morocco ilitangaza kuzinduliwa kwa mpango wa misaada siku ya Alhamisi kuwasaidia na kuwapatia tena makazi watu wa takriban majengo 50,000 yaliyoharibiwa na tetemeko baya la ardhi lililotokea Agosti 8.

Tetemeko la kiwango cha 6.8 kwa kipimo cha rikta– lilikuwa lenye nguvu kubwa sana ambalo halijawahi kutokea nchini Morocco -- limeua takriban watu 3,000 na kujeruhi zaidi ya 5,600 katika jimbo la Al-Haous, kusini mwa kiini cha utalii mjini Marrakesh.

Wale waliopoteza makazi watapewa makazi ya muda katika "majengo yaliyotengenezwa ili kuhimili hali ya mbaya ya hewa na baridi au katika maeneo ya mapokezi yenye vifaa vyote muhimu", ofisi ya ufalme ilisema katika taarifa kufuatia mkutano ulioongozwa na Mfalme Mohamed wa Sita.

Idadi ya watu waliopoteza makazi kutokana na tetemeko hilo, ambalo limeharibu vijiji vingi katika eneo la milima la Atlas nchini Morocco, haijulikani.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la Reuters