Rais wa Zimbabwe ameyasihi mataifa yanayolengwa na magharibi kuwa pamoja

Rais wa Iran, Ebrahim Raisi (L) na Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa wakiwa Harare, Zimbabwe

“Ni muhimu sana kwamba sisi, waathirika wa vikwazo vya Magharibi, tunazungumza wenyewe kwa wenyewe, tunawaonyesha kuwa tuko pamoja,” Mnangagwa aliwaambia waandishi wa habari baada ya mazungumzo na Raisi

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa ameyasihi mataifa yanayolengwa na vikwazo vya magharibi kuungana pamoja wakati akiwa mwenyeji wa kiongozi wa Iran, taifa jingine lililotengwa kimataifa.

Rais Ebrahim Raisi aliwasili katika kituo chake cha mwisho cha ziara ya kwanza Afrika, kufanywa na kiongozi wa Iran katika kipindi cha miaka 11, ziara ambayo imelenga kupunguza kutengwa kwa taifa hilo la Kiislamu.

Raisi ni kiongozi wa juu zaidi kuitembelea Zimbabwe katika kipindi muhimu cha kampeni za uchaguzi kwa ajili ya kura ya urais na wabunge inayoangaziwa kwa karibu hapo Agosti 23.

“Ni muhimu sana kwamba sisi, waathirika wa vikwazo vya Magharibi, tunazungumza wenyewe kwa wenyewe, tunawaonyesha kuwa tuko pamoja,” Mnangagwa aliwaambia waandishi wa habari baada ya mazungumzo na Raisi. “Nina furaha umekuja kuonyesha mshikamano,” Mnangagwa alimwambia Raisi alipowasili, akimwita “kaka yangu.”