Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 03, 2025 Local time: 11:56

Rais wa Iran akiwa Uganda amekemea vikali mwenendo wa Magharibi kuhusu ushoga


Rais wa Iran, Ebrahim Raisi. April 30, 2023.
Rais wa Iran, Ebrahim Raisi. April 30, 2023.

“Nchi za Magharibi leo zinajaribu kuhamasisha  wazo la ushoga na kwa kuhamasisha ushoga wanajaribu kumaliza kizazi cha binadamu,” Raisi alitangaza.

Rais wa Iran Ebrahim Raisi siku ya Jumatano alianzisha shutuma dhidi ya mwenendo wa mataifa ya magharibi kuhusu ushoga wakati wa ziara yake nchini Uganda, ambayo imepitisha baadhi ya sheria kali sana dhidi ya ushoga duniani.

Raisi, akiwa katika ziara ya kuimarisha uhusiano ambayo pia ni kwanza ya kiongozi wa Iran barani Afrika katika kipindi cha miaka 11, aliyakemea mataifa ya magharibi akiwa katika mkutano na waandishi wa habari, pamoja na Rais Yoweri Museveni baada ya mazungumzo na kiongozi huyo mkongwe wa Uganda.

“Nchi za Magharibi leo zinajaribu kuhamasisha wazo la ushoga na kwa kuhamasisha ushoga wanajaribu kumaliza kizazi cha binadamu,” Raisi alitangaza.

Museveni alitia saini mswaada huo kuwa sheria Mei 29, na kusababisha hasira miongoni mwa makundi ya haki za binadamu, Umoja wa Mataifa, na wanaharakati wa LGBTQ pamoja na mataifa ya magharibi.

Sheria hiyo mpya inafanya “ushoga uliozidi” kuwa kosa la jinai huku adhabu kwa mahusiano ya jinsia moja, ya kukubaliana, ni hadi kifungo cha maisha jela.

Forum

XS
SM
MD
LG