Rais wa zamani wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi, amefariki leo Alhamisi akiwa na umri wa miaka 98, vyanzo vya habari nchini Tanzania vimeeleza.
Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu, Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza siku saba za maombolezo kuanzia kesho kufuatia kifo chake.
Taarifa hiyo ya Ikulu ilisema marehemu Mwinyi alikuwa amelazwa hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.
Mwinyi alikuwa rais wa pili wa Tanzania kati ya mwaka 1985 na 1995.
Kabla ya kuchukua madaraka ya urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mwinyi alikuwa rais wa Zanzibar. Na pia alishika nyadhifa mbali mbali katika serikali ya Tanzania.