Erdogan, ambaye amekosoa vikali mashambulizi ya Israel huko Gaza dhidi ya Hamas, alianza kuzungumzia vita hivyo katika hotuba akipongeza sekta ya ulinzi ya nchi yake.
“Lazima tuwe na nguvu sana ili Israel isiendelei kufanya mambo haya ya kipuuzi kwa Palestina. Kama tulivyoingia huko Karabakh, kama tulivyoingia Libya, tunaweza kuwafanyia hilo hilo,” Erdogan aliuambia mkutano wa chama chake tawala cha AK katika mji alikozaliwa wa Rize.
“Hakuna sababu yoyote kwa nini hatuwezi kufanya hivyo. Lazime tuwe na nguvu ili tuweze kuchukua hatua hizo,” Erdogan aliongeza katika hotuba kupitia televisheni.
Rais Erdogan alionekana kutoa mfano wa hatua za miaka iliyopita zilizochukuliwa na Uturuki.
Mwaka 2020, Uturuki ilipeleka wanajeshi wake nchini Libya kuisaidia serikali ya Libya inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa.