Rais wa Madagascar akataa wito wa kusimamisha uchaguzi mkuu

Mgombea Urais wa Madagascar Andry Rajoelina akiwasalimu wafuasi wake huko Antananarivo, Novemba 3, 2018. REUTERS/Malin Palm

Timu ya rais anayemaliza muda wake nchini Madagascar Andry Rajoelina imeliambia shirika la habari la AFP siku ya Alhamisi kwamba rais huyo amekataa wito wa mkuu wa bunge wa kusimamisha uchaguzi wa rais utakaofanyika wiki ijayo wakati nchi hiyo inakabiliwa na mzozo wa kisiasa.

"Hakuna sababu kwa nini uchaguzi usifanyike Novemba 16," alisema msemaji wa Rajoelina, ambaye yeye mwenyewe anagombea kuchaguliwa tena katika uchaguzi huo Mkuu wa bunge la Madagascar siku y aAlhamisi alitoa wito wa kusimamishwa kwa uchaguzi wa rais wiki ijayo, baada ya wiki kadhaa za mikutano ya mara kwa mara ya upinzani.

Christine Razanamahasoa, ambaye anaongoza kikundi cha upatanishi kubuni njia ya kuumaliza mzozo wa kisiasa ambao umedumu kwa wiki kadhaa, alisema hali ya sasa nchini humo hairuhusu uchaguzi huru na wa kuaminika.

Kundi la upatanishi "limeidai vikali mamlaka kusimamisha uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika Novemba 16," Razanamahasoa aliuambia mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika mjini Antananarivo.

Lakini msemaji wa rais wa Madagascar anayemaliza muda wake Andry Rajoelina alilitaja ombi hilo kuwa "wazo la ajabu".

Taifa hilo la kisiwa cha Bahari ya Hindi limetikiswa na vita vikali vya kisiasa kati ya Rais Andry Rajoelina, anayewania kuchaguliwa tena na viongozi wengi wa upinzani.

Wagombea 11 kati ya 13 wa upinzani wamekuwa wakiongoza, maandamano yasiyoidhinishwa karibu kila siku mjini Antananarivo, kwa zaidi ya mwezi mmoja, wakipinga kile walichokiita "mapinduzi ya kitaasisi" ambayo yanampendelea rais aliyeko madarakani.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la AFP