Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 17, 2024 Local time: 21:43
VOA Direct Packages

Athari za vimbunga zaendelea kukumba wakazi wa Madagascar


Picha ya Satellite ikionyesha kimbunga Freddy kikielekea kugonga Madagascar. Februari 20. 2023. Reuters.
Picha ya Satellite ikionyesha kimbunga Freddy kikielekea kugonga Madagascar. Februari 20. 2023. Reuters.

Kufuatia kupigwa na vimbunga vitatu vikubwa ndani ya mwaka mmoja, Madagascar, inaendelea kushuhudia athari nyingi kutokana na hali hiyo kama vile njaa kwenye maeneo ya mashambani yasio fikiwa kwa urahisi, bila kupata misaada ya kimataifa, kulingana na makundi ya kutoa misaada ya kibinadamu.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, kimbunga Batsirai kiligonga taifa hilo Februari mwaka jana kikifuatiwa baada ya wiki mbili na kile cha Emnati, huku kile cha Freddy kikitua Februari mwaka huu.

Athari kutokana na vimbunga hivyo iliacha asilimia 60 hadi 90 ya maeneo ya ukulima kusini mashariki mwa kisiwa hicho yakiwa yameharibiwa, kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na UNICEF pamoja na ofisi ya kitaifa ya Lishe bora.

Matatizo yaliyojitokeza ni dhahiri kwa wakazi kama vile Lavosoa ambaye ni mama mwenye mtoto mchanga wa umri wa miezi 10 kwa jina Soaravo, ambaye huenda asifikishe mwaka mmoja kutokana na ukosefuwa lishe bora. Mama huyo pia ana mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 3, ambaye pia anasemekana kupungukiwa na lishe bora.

XS
SM
MD
LG