Rais Trump aweka ushuru wa asilimia 25 kwenye bidhaa za chuma kutoka nje

Rais Donald Trump akisaini amri ya kiutendaji inayoongeza ushuru kwenye bidhaa za chuma na aluminum, White House, Februari 10, 2025. Picha ya Reuters.

Rais Donald Trump Jumatatu alichukua hatua za kuongeza ushuru kwa kiasi kikubwa kwenye bidhaa za chuma na aluminum zinazoagizwa kutoka nje, na kufuta sheria iliyokuwa inaziruhusu Canada, Mexico, Brazil na nchi nyingine kuleta bidhaa hizo bila kulipa ushuru.

Trump alisaini amri ya kiutendaji ambayo inaongeza ushuru wa asilimia 25 kwenye aluminum badala ya ushuru wa awali wa asilimia 10 aliouweka mwaka 2018 ili kuokoa sekta hiyo inayodorora.

Hatua yake inarejesha ushuru wa asilimia 25 kwenye mamilioni ya tani za bidhaa za chuma na aluminum zilizokuwa zinaagizwa nje na kuingia Marekani chini ya makubaliano ya kutolipisha ushuru bidhaa hizo.