Rais Samia aongoza viongozi wa mataifa kuuaga mwili wa Hayati Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akitoa heshima za mwisho kwenye jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu ya tano hayati John Pombe Magufuli katika uwanja wa Jamhuri Dodoma. Picha na Ofisi ya Rais.
Rais wa Zanzibar Hussein Ali Mwinyi akitoa heshima za mwisho kwenye jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Hayati John Pombe Magufuli katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma. Picha na Ofisi ya Rais.
Rais wa Jamhuri ya Watu wa Kenya Uhuru Kenyatta akitoa heshima za mwisho kuuaga Mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hayati John Pombe Magufuli kwenye mazishi ya kitaifa yaliyo fanyika leo Machi 22, 2021, Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC Felix Tshisekedi akitoa heshima za mwisho kwenye jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu ya tano Hayati John Pombe Magufuli katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Baadhi ya mabalozi kutoka mataifa mbalimbali Duniani walioshiriki kwenye ghafla ya mazishi ya kitaifa ya kuuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hayati John Pombe Magufuli, wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Makamanda wa JWTZ wakipiga saluti mara baada ya kuweka jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu ya tano ya hayati John Pombe Magufuli katika chumba maalumu kwa ajili ya shughuli ya kuagwa na viongozi mbalimbali.
Gari Maalumu la Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ likiwa limebeba jeneza lenye Mwili wa Aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Hayati John Pombe Magufuli wakati likiwasili katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma. Picha na Ofisi ya Rais.
Gari Maalumu la Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ likiwa limebeba Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano hayati John Pombe Magufuli wakati likiwasili katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma. Picha Ofisi ya Rais.
Gari Maalumu la Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ likiwa limebeba Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu ya tano Hayati John Pombe Magufuli wakati likiwasili katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.