Nchi za Magharibi zilizuia dola bilioni 300 za mali za kifedha za Russia, hasa zile za akiba ya benki kuu, baada ya Moscow kupeleka wanajeshi kuivamia Ukraine mwezi Februari 2022.
Na bunge la Marekani mwezi uliopita lilipitisha mswaada unaomruhusu Rais Joe Biden kutumia mali zilizokamatwa za Russia nchini Marekani kwa ajili ya mfuko maalum wa kuisaidia Ukraine.
Amri hiyo ya Russia itazipa haki kampuni za Russia, mashirika na watu binafsi walioathiriwa na vikwazo, haki ya kuomba fidia kutoka katika serikali ya Russia.
Fidia hiyo itatoka kwenye mali zinazomilikiwa na Marekani, kama majengo, akaunti za benki na hisa, zilizopo nchini Russia.
Kampuni nyingi za nchi za Magharibi ziliondoka nchini Russia tangu ilipoanzisha uvamizi dhidi ya Ukraine.