Rais Kiir azuru Ethiopia

Mkutano wa IGAD, Ethiopia

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amewasili Addis Ababa kwa ziara ya siku moja.

Rais amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia Workneh Gebeyehu katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ababa Bole.

Shirika la habari la serikali ya Ethiopia limeripoti kuwa wakati akiwa Ethiopia, rais huyo anatarajiwa kukutana na kuzungumza na Waziri Mkuu Abiy Ahmed juu ya juhudi za kuleta amani Sudan Kusini.

Baraza la Mawaziri la Mamlaka inayoshirikisha serikali katika maendeleo (IGAD) linatarajiwa kuendesha kikao cha kisicho cha kawaida Addis Ababa Alhamisi ili kujadili adhabu zinazotakiwa kutolewa kwa wale wanaovunja amani nchini Sudan Kusini.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pia linatarajiwa kupiga kura Alhamisi (Mei 31) kuweka vikwazo dhidi ya maafisa wa ngazi ya juu wa serikali ya Sudan Kusini.