Biden anatarajiwa kutoa hotuba yake ya kwanza kama rais Alhamisi, akitumia hotuba hiyo kujadili msaada huo pamoja na athari zake kwa wananchi wa Marekani kuelekea mbele na kuzungumzia mwaka uliopita ambapo COVID-19 imeua zaidi ya watu 529,000 na kuambukiza watu wapatao milioni 29 nchini Marekani.
Muswada huo ulipitishwa kupitia baraza la Seneti na Baraza la Wawakilishi ambayo yote yanadhibitiwa na Wademokrat bila uungaji mkono wa Warepublican.
Kura za maoni ya umma hivi karibuni zimeonyesha kwamba kwa jumla mswaada unungwa mkono na watu wengi ingawa wengi wao ni wanaounga mkono chama cha demokrat kuliko wale wanaotambulika kama Warepublican.
Msaada huo ni pamoja na fedha kiasi cha dola 1,400 kwa mamilioni ya wamarekani na msaada kwa waliopoteza ajira na mabilioni ya dola kusaidia majimbo na serikali za mitaa na biashara ambazo zimeathiriwa kiuchumi na janga la corona.
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Sunday Shomari, Washington, DC.