Rais Biden arejea Marekani baada ya kukamilisha ziara Angola

Rais wa Marekani Joe Biden akifurahia ngoma ya asili ya watu wa Angola baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Catumbela Angola, Dec. 4, 2024.

Rais wa Marekani Joe Biden amerejea nchini mapema leo akitua katika uwanja wa Andres Airforce Base  katika jimbo la Maryland akitoeka nchini Angola.

Wakati wa ziara yake rasmi , rais Biden aliahidi msaada mwingine wa dola milioni 600 jumatano kwa mradi mkubwa wa reli wa nchi kadhaa barani Afrika kama moja ya sera ya mwisho ya mambo ya nje chini ya utawala wake. Aliwaambia viongozi wa Afrika kwamba bara lenye rasilimali nyingi na zaidi ya watu bilioni 1.4 limeachwa nyuma kwa muda mrefu.

Rais wa Marekani akiwa na viongozi wengine wa Afrika katika eneo la bandari ambapo ujenzi wa miundombinu ya kupokea mizigo inajengwa, huko Lobito, Angola, Jumatano, Disemba 4, 2024.

Biden alitumia siku yake ya mwisho kuitembelea Angola katika ziara iliyosubiriwa kwa muda mrefu katika nchi zilizo chini ya jangwa la sahara, kama rais na Kwenda hadi mji wa mwambao wa LOBITO na kutembelea kituo cha bandari cha Atlantiki ambacho ni sehemu ya uundaji upya wa reli ya Lobito Corridor.

Hata hivyo Biden ameelezea kama uwekezaji mkubwa katika mradi wa reli nje ya Marekani.