Maelfu ya waandamanaji waingia uwanja wa Tahrir kudai mabadiliko baada ya Mubarak kujiuzulu.
Maelfu ya Wamisri wameingia mitaani katika nchi nzima ya Misri kukupinga kile walichokiita kasi ndogo ya mabadiliko ya serikali na kucheleweshwa kuwafungulia mashitaka maafisa wa zamani wanaohusishwa na mauaji ya ya waandamanaji wanaounga mkono demokrasia.
Waandamanaji walijaa leo kwenye uwanja wa Tahrir katika moja ya maandamano makubwa tangu upinzani wa siku 18 uliopelekea kujiuzulu kwa rais wa zamani Hosni Mubarak mwezi February.
Wanaharakati wameweka mahema kwenye uwanja ambapo wamisri wanaimba na kuinua bendera zao.