Raia wa Haiti watoa hisia mseto kuhusu amri ya kutotoka nje

Watoto wakiwa katika kituo cha muda kilichowekwa kwa ajili ya familia zilizo lazimika kukimbia makazi yao kutokana na ghasia za magenge ya uhalifu huko Port-au-Prince, Haiti, Machi 13, 2024.

Milio ya risasi ilisikika huko Port-au-Prince baada ya siku tatu za utulivu wa kiasi, wakati ambapo mazungumzo ya kuundwa kwa mamlaka ya mpito yanaendelea kujaribu kuiondoa nchi hiyo ya Caribbean kutoka katika mgogoro wake mkubwa wa kisiasa .

Serikali inayoondoka madarakani iliongeza muda wa amri ya kutotoka nje usiku hadi Jumapili katika jimbo la Magharibi, ambalo linajumuisha mji mkuu.

Waziri Mkuu wa Haiti aliyetangaza kujiuzulu Ariel Henry

Wakati wa mkutano wa dharura nchini Jamaica na ushiriki wa wawakilishi wa Haiti, Jumuiya ya Mataifa ya Karibean (Caricom), Umoja wa Mataifa na nchi kadhaa kama vile Marekani na Ufaransa ziliyapa majukumu makundi ya Haiti kuanzisha Baraza la mpito wa kitaifa.

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa ambavyo vimeongea na shirika la AFP , Baraza hilo limetakiwa lijumuishe wapiga kura saba wanaowakilisha wakuu wa siasa nchini Haiti na sekta binafsi.

Aidha baraza hilo limetakiwa kuchagua waziri mkuu wa muda ambaye atateua serikali itakayo jumuisha wengine. Makundi sita kati ya saba yamewasilisha jina la mwakilishi wao kwa Caricom,