Pompeo ahudhuria mazungumzo Ugiriki kujadili mvutano kati ya Athens na Ankara

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo anaanza mazungumzo huko Ugiriki ya kupunguza mvutano wa mashariki mwa Mediterranean na kuongeza juhudi mbadala kwenye mashauriano baina ya Athens na Ankara.

Pompeo anaanza ziara yake ya siku mbili kwa mkutano na viongozi wenzake wa Ugiriki, Nikos Dendias huko Thessaloniki. Hakuna upande wowote uliotoa taarifa za mkutano wao.

Wanachama hao wawili wa NATO wanavutana juu ya uchunguzi wa nishati katika eneo la maji yenye mabishano, baada ya Ankara kuongeza utafiti wa Hydrocarbon baharini.

Mvutano huo umeyaingiza mataifa mengine ya Ulaya, na kuongeza wasiwasi wa kusambaa zaidi.

Lakini wiki iliyopita, Athens na Ankara walisema walikuwa tayari kuanza mazungumzo.

“Tukutane tuzungumze na tutafute suluhisho linalokubalika kwa pande zote. Tuipe nafasi diplomasia, Mitsotakis alisema Ijumaa kwa Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, katika hotuba yake kwa baraza kuu la Umoja wa Mataifa.

Kabla ya safari hiyo, ofisa mwandamizi wa Marekani alisema Washington ilikuwa na nia ya kupunguza mvutano huo, uwezekano wa ajali au matukio” na kwa Ugiriki na Uturuki ili kukamilisha makubaliano.

Nchi hizi mbili hazikubaliani juu ya mipaka yao katika bara hilo, miongoni mwa masuala mengine mbali mbali.

Tangu wakati huo Uturuki imeikumbuka meli yake ya Oruc Reis, na Athens na Ankara walitangaza wiki iliyopita wamekubali kuanzisha tena mazungumzo, hatua iliyokaribishwa na Marekani ambayo imeshawishi mazungumzo hayo.

Ni mara ya kwanza, waziri wa mambo ya nje wa Marekani kutembelea Thessaloniki, inayoonekana kama lango la uwekezaji na biashara huko Balkan.

Wakimbizi na wahamiaji wakiwasili kwenye mji wa Thessaloniki, kaskazini mwa Ugiriki

Pompeo amesaini makubaliano ya pande mbili ya sayansi na teknolojia wakati akiwa Ugiriki, ambayo inataka kuwa kitovu cha nishati katika nchi za Balkan, na kukutana na viongozi wa biashara katika sekta ya nishati.

Kesho Jumanne, Pompeo atafanya mazungumzo na Mitsotakis katika kituo cha kijeshi cha Souda, kituo cha majeshi ya NATO na Ugiriki katika kisiwa cha Krete.

Mitsotakis, ambaye ni mwenyeji wa Pompeo, nyumbani kwake huko Krete, anataka uhusiano wa karibu wa kijeshi na Marekani.waziri wa mambo ya nje alisaini makubaliano ya ulinzi hapo Oktoba mwaka uliopita, akiruhusu vikosi vya Mrekani kuwa na matumizi mapana katika vituo vya jeshi la Ugiriki.

Jambo muhimu katika makubaliano ya Oktoba, ilikuwa bandari ya kaskazini ya Ugiriki ya Alex-androupolis, lango la Balkan na Black Sea lenye thamani ya kimkakati kwa jeshi la wanamaji la Marekani na NATO.

Marekani imepewa kipaumbele kwa bahari hiyo, baada ya kulipa takribani dola milioni 2.3, kuondoa majahazi yaliyozama ambayo yalizuia sehemu ya bandari hiyo tangu mwaka 2010.

Wakati huo maafisa wa Ugiriki walisema Pentagon, ilitarajiwa kuwekeza zaidi yad ola milioni 14, kwenye uwanja wa ndege wa Ugiriki wa Larissa na karibu Euro milioni sita huko Marathi, sehemu ya kituo cha Souda.