Tawi la vijana wa Chadema lilikuwa limetangaza siku ya Jumamosi kwamba vijana wapatao 10,000 walitarajiwa kukutana katika mji wa kusini magharibi wa Mbeya kuadhimisha siku ya kimataifa ya vijana leo Jumatatu chini ya kauli mbiyu “chukua udhibiti wa mstakabali wako.”
Lakini Awadh Haji, mkuu wa polisi anayehusika na operesheni na mafunzo, alisema jeshi la polisi “limeona ishara za wazi kwamba lengo lao sio kuadhimisha siku ya kimataifa ya vijana bali kuanzisha na kushiriki katika vurugu.”
Taarifa yake ilitoa mfano wa vijana wa Kenya, ikionekana kumaanisha wiki kadhaa za maandamano ya kuipinga serikali katika nchi jirani ya Afrika Mashariki yaliyoongozwa kwa kiasi kikubwa na vijana.
“Polisi waliamua kupiga marufuku mkutano wa aina yoyote wa ndani na wahadhara au maandamano ambayo yamepangwa kufanyika chini ya jina la kuadhimisha siku ya vijana,” Haji alisema, akionya kuwa yanaweza kusababisha kuvurugika kwa amani.
Maafisa wa chadema wamelaani uamuzi huo, na kumtaka Rais Samia Suluhu Hassan kuingilia kati, wakiituhumu polisi kwa kujaribu kuzuia misafara ya magari inayoelekea Mbeya na kuwakamata baadhi ya vijana.