Wakati huohuo Polisi wa Israel wameitisha vikosi vya ziada vya usalama kuulinda mji wa Jerusalem kufuatia tangazo la Rais wa Marekani Donald Trump kuwa Jerusalem ni mji mkuu wa Israel na Marekani ina mpango wa kuhamisha ubalozi wake katika mji huo.
Siku za nyuma, Israel ilikuwa imeweka katazo kwa watu wa umri fulani kuingia katika Hekalu la Mount Jerusalem ambapo uvunjifu wa amani umekuwa ukitokea wakati kuna migogoro.
Msemaji wa Israeli Mickey Rosenfeld amesema, “Hatuna fununu yoyote kuwa kutakuwa na fujo katika eneo la mount na hivyo hakuna kipangamizi cha umri. Kama kutakuwa na machafuko tutachukua hatua mara moja.”
Eneo hilo linajulikana na Waislam kama ni eneo takatifu na pia kwa Mayahudi ni Hekalu la Mount. Ni eneo takatifu la Mayahudi na eneo la tatu takatifu kwa Waislam.
Maadamano yanaendelea kufanyika Ijumaa kote Mashariki ya Kati na katika nchi zenye Waislam wengi (kufuatia kutangazwa Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel na Marekani0.