Papa Francis atembelea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo akiwa na ujumbe wa amani.

  • Abdushakur Aboud

Papa Francis awasalimu watoto alipokuwa anakutana na wajumbe wa mashirika ya hisani katika kanisa la Apostolic Nunciature mjini Kinshasa, DRC

Papa Francis anamuombea dua muathirika wa vita vya mashariki ya Congo.

Papa Francis akiwa kwenye gari lake dogo akiwasili kwenye uwanja wa Ndolo ili kuongoza misa mjini Kinshasa.

Papa Francis aongoza misa iliyohudhuriwa na karibu watu milioni moja mjini Kinshasa, DRC

Papa Francis awasili kwenye uwanja wa Ndolo kuongoza misa , mjini Kinshasa, DRC.

Umati wa watu kwenye uwanja wa Ndolo wakihudhuria misa inayongozwa na Papa Francis mjini Kinshasa, DRC

Waumini waliokusanyika ndani ya uwanja wa Ndolo kwa misa maalum iliyoongozwa na Papa Francis.

Watu ambao hawakuweza kuingia ndani ya uwanja wa Ndolo ambako Papa Francis anaongoza misa.

Watoto wanaimba wakimkaribisha Papa Francis kwenye uwanja wa Ndolo.

Papa Francis akutana na waumini kwenye kanisa la Apostolic Nunciature, mjini Kinshasa.

Papa Francis aliwasili Kinshasa Jumanne Januari 31, na kutoa wito kwa Jumuia ya Kimataifa kutojihusisha ndani ya masuala ya Afrika, na kuwaachia waafrika watanzuwe matatizo yao wenyewe.