Afisa mmoja aliyezungumza kwa masharti ya kutotajwa alisema baba mtakatifu alitangaza hatua hiyo wiki iliyopita mbele ya wasaidizi wake wa juu kwenye mkutano wa kawaida wa Vatican.
Alimnukuu baba mtakatifu akisema, Burke mmoja wa wakosoaji wake wakubwa, anafanya kazi dhidi ya kanisa na papa” na kwamba alisababisha mfarakano katika kanisa.
Burke amekuwa hana kazi ya juu Vatican kwa miaka mingi. Yeye ni mshauri wa moja ya mahakama zake kama vile makadinali wengi wanaoishi nje ya Roma na anatumia muda wake mwingi katika jimbo lake la asili la Wisconsin.
Hii ni hatua ya pili kwa baba mtakatifu kuchukua ambapo Novemba 11 alimwondoa Askofu Joseph Strickland wa Tayler , Texas, mkosoaji mkonservative , baada ya kukataa kujiuzulu kufuatia uchunguzi wa Vatican kuhusu uongozi wake katika dayosisi.
Chanzo cha habari hii ni VOA News.