Papa Francis aliakhirisha mkutano wake na waumini wa asubuhi siku ya Jumamosi kwa sababu ya flu, Vatican ilisema katika taarifa.
Papa huyo mwenye umri wa miaka 86 hufanya mikutano ya mara kwa mara na maafisa wa Vatican siku za Jumamosi pamoja na hadhira za kibinafsi.
Mapema mwezi huu, Papa aliahirisha kusoma hotuba iliyotayarishwa kwa ajili ya mkutano na marabii wa Ulaya kutokana na homa lakini alionekana kuwa na afya njema wakati wa mkutano na watoto saa chache baadaye.
Forum