Uamuzi wa Trump wampa wasiwasi Papa Francis

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza Boris Johnson

Wakati Rais Donald Trump akijiandaa kutangaza Marekani inaitambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israeli na itahamisha ubalozi wake kutoka Tel Aviv viongozi kadhaa wameeleza wasiwasi wao.

Viongozi hao duniani akiwemo Papa Francis wameeleza “wasiwasi wao mkubwa” kutokana na uamuzi huo.

Kwa upande wake Uturuki imeitisha mkutano wa Umoja wa ushirikiano wa nchi za Kiislam (OIC) Jumatano ili kuratibu majibu ya pamoja juu ya uamuzi huo.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu hakutaja suala hilo alipotoa hotuba yake kwa uma Jumatano.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza Boris Johnson amesema nchi yake haina mapango wakuhamisha ubalozi wake Tel Aviv.

“Tunachukulia ripoti hizo tulizozipata kwa wasiwasi kwa sababu tunafikiria kuwa Jerusalem bila shaka ni lazima iwe ni sehemu ya kufikia suluhu yoyote itakayofanyika baina ya Israeli na Palestina—mazungumzo ya kutafuta makubaliano ambayo tunataka kuona yakanyika,” Johnson amesema.

Mataifa ya Kiarabu na Kislamu yameonya kwamba uwamuzi wowote wa kuhamisha ubalozi wa Marekani utachochea mvutano mkubwa katika kanda hiyo na kuharibu juhudi za marekani za kupatikana makubaliano ya Amani kati ya Israel na waarabu.

Hata hivyo, ikulu ya White House imesema kwamba anachofanya Trump, ni kutambua ukweli wa mambo na ukweli wa kihistoria.

Kabla ya kutoa tangazo lake Trump aliwapigia simu viongozi watano wa Mashariki ya Kati, kuwaelezea kuhusu hatua hiyo.

Hata hivyo, Ikulu hiyo ilitoa maelezo machache tu, kuhusu yaliyojadiliwa kwenye mazungumzo hayo na viongozi hao.