Papa Francis alisema hayo wakti akijumuisha suala la biashara ya ujauzito, kwenye hotuba yake ya kila mwaka, ilioangazia tishio lililopo kwa Amani ya dunia, pamoja na hadhi ya binadamu.
Wakati wa hotuba ya sera za kigeni kwa mabalozi waliopo Vatican, Francis amelalamika kwamba mwaka 2024 umeanza wakati Amani ikiwa imetishiwa, kudhoofishwa au hata katika baadhi ya sehemu, kupotea kabisa. Akiangazia vita vya Russia na Ukraine, Israel na Hamas, uhamiaji, mabadiliko ya hali ya hewa pamoja na utengenezaji haramu wa silaha za nyuklia na silaha zingine hatari.
Aliendelea kuelezea orodha ya baadhi ya mambo yanayoathiri ubinadamu na kuongezeka kwa ukiukaji wa sheria za kimataifa za kibinadamu unaopelekea hali hiyo.