Mamlaka nchini Norway ilisema walinzi wa mpakani walimkamata karibu na mpaka wa Russia na Norway mapema Ijumaa.
Wakili wa Medvedev ameyaambia mashirika ya habari kuwa Medvedev alikuwa Norway akiomba hifadhi.
“Alitangaza kuwa yuko tayari kuzungumzia kile alichokishuhudia wakati akifanya kazi na kampuni ya Wagner Group, dhidi ya watu wanaochunguza uhalifu wa kivita” wakili Brynjulf Risnes alisema.
Maafisa wa Ukraine walisema Jumanne, idadi ya vifo kutokana na shambulizi la kombora kwenye jengo la makazi katika mji wa Dnipro, iliongezeka na kufikia 41 baada ya waokoaji kupata mwili wa mtoto uliokuwa umefukiwa katika kifusi.
Gavana wa mkoa Valentyn Reznichenko amesema watu 25 bado hawajulikani walipo huku asilimia 90 ya kifusi ikiwa imeondolewa. Ameongeza kuwa watu 79 wamejeruhiwa katika shambulizi hilo na 28 kati yao wamelazwa hospitali.
Raisi wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amesema katika hotuba yake ya kila usiku, Jumatatu kuwa shambulio la Dnipro linaonyesha haja kwa maamuzi ya haraka na yaliyoratibiwa zaidi kuhusiana na upelekaji wa silaha nchini Ukraine.
Chanzo cha habari hii kinatokana na mashirika mbalimbali ya habari