Bei ya mafuta iliongezeka Jumatano kwenye vituo vya mafuta kote nchini Nigeria, likiwa pigo lingine kwa raia wa Nigeria ambao tayari wanakabiliwa na mzozo mbaya wa kiuchumi katika miongo kadhaa.
Kampuni ya mafuta ya serikali haijatoa maelezo kuhusu kupanda huko gafla kwa bei ya mafuta ambayo imeongezeka kati ya asilimia 15 na asilimia 20 kwenye vituo vya mafuta kote nchini.
Lakini ni ongezeko la pili katika kipindi cha mwezi mmoja, na mapema mwezi Septemba, kampuni ya taifa ya mafuta (NNPC) ilikiri kuwa ina madeni makubwa kwa wanaoiuzia mafuta na ilitangaza ongezeko la bei la asilimia 40 ili kuinua hazina yake.
Wanigeria tayari wanakabiliana na mfumko mkubwa wa bei na gharama ya chakula, vile vile mdororo wa sarafu ya naira.