Mzozo wa Misri na Ethiopia juu ya bwawa la Nile wachukua sura mpya

Bwawa la Nile ambalo limejengwa na Ethiopia.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri wa masuala ya Afrika ameishutumu Ethiopia kwa kuvuta muda wa mashauriano  huku ikiendelea kujaza maji kwenye bwawa lake  la Nile linalozozaniwa bila kuwa na makubaliano.

Katika taarifa ya Jumatano waziri huyo ameshutumu taarifa za Ethiopia ambazo zimeilaumu Cairo kuingiza siasa katika mzozo wa bwawa la Nile.

Mzozo huo mpya ulizua maoni tofauti katika vyombo vya habari vya Misri.

Mtangazaji maarufu anayeiunga mkono serikali Ahmed Moussa alisema Addis Ababa ilijenga kwa makusudi bwawa kubwa la kufua umeme Ethiopia ili kuzidhuru Misri na Sudan.

Mtangazji wa televisheni ya upinzani Mohammad Nasser aliilaumu serikali ya Msiri na vyombo vya habari kwa kutochukua msimamo mkali zaidi dhidi ya suala hilo.

Ethiopia, Sudan, na Misri zimekuwa katika mzozo kwa muda mrefu kufuatia bwawa hilo, ambapo Sudan na Misri zinahofia itapunguza nafasi yao ya matumizi ya maji kutoka kwenye mto Nile.