Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 15:47

Waziri Mkuu wa Ethiopia ameapa kuvivunja vikosi vvya kikanda vyenye nia ya uharibifu


Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed

Mpango huo uliotangazwa kwa mara ya kwanza Alhamisi unalenga kuunganisha vikosi kama hivyo ambavyo vilianzishwa kwa upande mmoja na baadhi ya mikoa na kuviingiza katika jeshi la serikali kuu, polisi wa mkoa, au maisha ya kiraia

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed ameapa Jumapili kuvivunja vikosi vya kikanda vilivyoundwa na baadhi ya mikoa akionya hatua za utekelezaji zitachukuliwa dhidi ya upinzani wowote wenye nia ya uharibifu.

Mpango huo uliotangazwa kwa mara ya kwanza Alhamisi unalenga kuunganisha vikosi kama hivyo ambavyo vilianzishwa kwa upande mmoja na baadhi ya mikoa na kuviingiza katika jeshi la serikali kuu, polisi wa mkoa, au maisha ya kiraia. Vikosi hivi vimezua utata siku za nyuma hususani wakati wa vita vya kikatili vya Tigray huku maafisa wa usalama wanaoendesha shughuli zao katika mkoa wa Amhara wakituhumiwa kwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu.

Katiba ya Ethiopia inaruhusu serikali za mikoa 11 zilizoundwa katika misingi ya lugha na utamaduni kuendesha vikosi vyao vya polisi vya kikanda.

XS
SM
MD
LG