Kikosi cha Ukombozi cha Watu wa Tigray (TPLF), ambacho kiliongoza eneo la kaskazini kwenye vita na serikali kuu mwishoni mwa 2020, kilitajwa kama kikundi cha kigaidi Mei 2021.
Mzozo huo ulimalizika kwa mapatano yaliyotiwa saini mjini Pretoria Novemba mwaka jana baada ya maelfu ya watu kuuawa na mamilioni kulazimishwa kukimbia makazi yao.
Bunge la Ethiopia limesema katika taarifa yake kwamba wabunge wengi wameunga mmono kufutwa kwa orodha hiyo.
Kufutwa kwa orodha hiyo ni sharti la ushiriki wa jeshi la TPLF katika serikali ya mpito ambayo chama hicho kilimteua msemaji wake Getachew Reda wiki iliyopita kukiongoza.
Getachew hakujibu mara moja ombi la maoni siku ya Jumatano.
Dessalegn Chanie, mbunge kutoka chama cha upinzani cha National Movement of Amhara (NAMA) alipiga kura ya kupinga kuondolewa huko akiishutumu TPLF kwa kutotekeleza ahadi zake katika mkataba wa amani.