Albamu yake ya kwanza ya Loliwe ghafla ilimfanya Zahra kuwa mvuto lakini inasemekana katika miaka ya hivi karibuni amekuwa akisumbuliwa tatizo la unywaji pombe.
Zahara alizaliwa Bulelwa Mkutukana, alikuwa amelazwa hospitali tangu mwezi uliopita na familia yake imesema katika taarifa iliyotolewa kupitia mtandao wa Instagram kuwa Zahara alifariki usiku wa Jumatatu “akiwa amezunguukwa na familia na jamaa zake”
“Kipaji kikubwa cha Zahara katika uimbaji na mapenzi aliyekuwanayo kwenye mziki ameyagusa maisha ya mamilioni ya watu” taarifa hiyo iliongeza.
Zahara anajulikana kwa upigahi gitaa wake na mtindo wake wa nywele wa Afro, alizaliwa katika kijiji maskini jirani na East London huko Afrika Kusini.
Alipokuwa mtoto aliimba kwaya na kujifunza kupiga gitaa. Sauti yake ililingamishwa na ya Tracy Chapman, Joan Armatrading na India Arie.
Albamu yake ya kwanza mwaka 2011 iliuzwa ndani ya saa 72 na ghafla ilimbadilisha kuwa mwimbaji nyota wa Afrika.
Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la AFP