Mwandishi wa Korea Kusini Han Kang amepewa tuzo ya Nobel katika uandishi wa fasihi kutokana na mashairi yake yanayoangazia uhalisi wa kihistoria na kufichua matatizo ya maisha yanayomkumba binadamu.
Riwaya yake ya "The Vegetarian" ilishinda tuzo ya kimataifa ya Booker mwaka 2016.
Mwandishi huyo ni wa 221 kupewa tuzo hilo yenye thamani kubwa sana katika ulimwengu wa fasihi.
Tuzo ya Nobel ya fasihi imekuwa ikitolewa tangu mwaka 1901
Kwa muda wa miongo kadhaa iliyopita, tuzo ya Nobel kwa ajili ya waandishi ilikuwa ikishindwa na wazungu.
Lakini sasa wasio wazungu wamekuwa wakishinda, ikiwemo kutoka Misri, Nigeria, Mexico, Japan na Marekani.