Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Oktoba 11, 2024 Local time: 11:22

Wanasayansi waliogundua chanjo ya Covid washinda Tuzo ya Nobel ya Dawa ya 2023


Wanasayansi Katalin Kariko (Kushoto) Dkt Drew Weissman, washindiwa tuzo ya Nobel ya Dawa mwaka 2023.
Wanasayansi Katalin Kariko (Kushoto) Dkt Drew Weissman, washindiwa tuzo ya Nobel ya Dawa mwaka 2023.

Tuzo ya Nobel ya Dawa mwaka huu imetolewa kwa wanasayansi wawili kutokana na uvumbuzi wao wa chanjo za Covid aina  ya mRNA.

Kamati inayotoa tuzo hizo imesema kwamba Kataline Kariko na Drew Weissman walipiga hatua muhimu wakati wa janga la corona. Kariko ni profesa kwenye chuo kikuu cha Szeged, na pia kwenye chuo cha afya cha Perelman katika chuo kikuu cha Pennsylvania.

Weissmana ni profesa kwenye chuo cha utafiti wa chanjo cha Roberts Family na pia mkurugenzi kwenye chuo cha RNA Innovations cha Pennsylvania. Tuzo ya Nobel ya Dawa siku zote huwa ya kwanza kutolewa miongoni mwa nyingine kila mwaka.

Tuzo za fizikia, kemia, fasihi, amani na uchumi zitatangazwa kila siku hadi Okotoba 9. Alfred Nobel mwanzilishi wa tuzo hizo alikuwa mfanyabiashara katika karne ya 19 na ambaye alijipatia utajiri mkubwa baada ya kugundua dynamite. Tuzo ya kwanza ya Nobel ilitolewa 1901 miaka 5 baada ya kifo chake.

Forum

XS
SM
MD
LG