Mwanaharakati wa upinzani nchini Iran Nader Afshari amekamatwa nchini Iran kwa kujihusisha na maandamano ya kupinga serikali ya Iran.
Mama wa mpinzani huyo wa Iran amesema afisa mmoja wa mahakama alimwambia kwamba mtoto wake wa kiume alikuwa miongoni mwa watu kadhaa waliokamatwa.
Watu hao wamekamatwa kwa kujihusisha na maandamano ya kupinga serikali yaliofanyika wiki iliyopita karibu na Tehran.
Katika mahojiano ya simu na VOA siku ya Jumatano Maryam Sabzeparvar alisema amefahamu kukamatwa kwa Afshari wakati alipozungumza na maafisa katika mahakama ya mapinduzi katika mji wa Karaj siku moja kabla.
Amesema ugunduzi wake ulikuja baada ya siku kadhaa za kujaribu kufahamu juu ya nini kilimtokea mwanae mwanaharakati wa haki za binadamu aliyepotea wakati wa maandamano ya kupinga serikali huko Karaj Agosti moja.