Mlipuko wa Jumapili ulikuwa wa pili kulikumba soko maarufu la Bakara katika muda wa mwezi mmoja tu.
Ni soko kubwa sana mjini Mogadishu na ambako wakazi wengi hupata mahitaji yao ya vyakula, nguo, dawa, vifaa vya elektroniki na vitu vingine.
Wafanyakazi wa zima moto waliwasili kuzima moto huku wakaazi na wamiliki wa biashara kama Mohamed Abdi wakitazama.
Mamlaka ilisema inaamini kuwa kilipuzi kilikuwa kimewekwa karibu na soko.
Haijabainika mara moja ni nani aliyehusika ingawa kundi la wanamgambo la Al-Shabaab mara kwa mara hutekeleza mashambulizi ya mabomu nchini Somalia.
Kundi hilo limekuwa likipambana na serikali ya Somalia na kikosi cha ulinzi wa amani cha Umoja wa Afrika kwa miaka mingi