Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 06:48

Cuba yachukua hatua za dharura kufahamu hatma ya madaktari wake walotekwa nyara.


Spika wa bunge la Cuba Esteban Lazo akiwa Havana Aprili 18, 2018. Picha na HO / www.cubadebate.cu / AFP.
Spika wa bunge la Cuba Esteban Lazo akiwa Havana Aprili 18, 2018. Picha na HO / www.cubadebate.cu / AFP.

Spika wa bunge la Cuba Esteban Lazo anatembelea Nairobi kwa lengo la kupata maelezo bayanajuu ya hatma ya madaktari wawili wa Cuba waliotekwa nyara nchini Kenya na wanamgambo wa Somalia takriban miaka mitano iliyopita.

Katika taarifa wizara ya mambo ya nchi za nje mjini Havana, inaeleza kwamba ziara ya mjumbe maalum Lazo unafanyika baada ya Al-Shabab kutoa taarifa ya Al- Shabaab kwamba madaktari hao wawili wameuawa kutokana na shambulio la anga la Marekani wiki iliyopita.

Lazo “amekwenda Kenya kwa lengo la kushiriki katika utaratibu wa dharura na maafisa waandamizi wa nchi hiyo,“ imeleza taarifa ya wizara iliyochapishwa Junanne.

Spika huyo wa Bunge “anataka ushirikiano na ufafanuzi, kutoka wakuu wa Nairobi, kwa kuzingatia habari za hivi karibuni zilizochapishwa kuhuhusu uwezekano wa vifo ambavyo havikuthibitishwa vya madaktari Assel Herrera Correa na Landy Rodriguez Hernandez ambao walitekwa nyara nchini humo April 12, 2019.

Taarifa hivyo haikutoa maelezo zaidi kuhusu safari yake.

Kundi hilo la wanamgambo wa Kiislamu lenye ushirikiano na Al-Qaeda limesema madaktari hao wawili waliuawa katika mashambulizi kadhaa ya ndege zisizo na rubani” katika mji wa kusini wa Somalia wa Jilib hapo Februari 15.

Madai hayo hayakuweza kuthibitishwa kwa njia huru.

Makao makuu ya jeshi la Marekani barana Afrika, katika taarifa siku ya Jumatatu, imethibitisha kuwa shambulio la anga lililenga vituo kadhaa vya Al-Shabaab karibu na Jilib siku hiyo.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP

Forum

XS
SM
MD
LG